Change Agents The Podcast
Reparations Media & Juneteenth Productions
Are YOU a “Change Agent”? Organizer. Activist. Educator. Policy maker. Block club leader. Nonprofit founder. Religious leader. Business owner. Voter. Neighbor.
Change Agents is a documentary series revealing the power of community-driven activism told by those in the fight. These are the stories you aren’t hearing — told by and for communities of color and other marginalized communities that have long been overlooked, misrepresented and maligned.
Headquartered in Chicago and produced across the Midwest, we highlight authentic, actionable, grassroots solutions to society’s most pressing problems — including reentry after incarceration, homeownership disparities, anti-Blackness, the mental health crisis, and more.
Produced by a team made up of BIPOC, female, queer and disabled journalists, for Reparations Media, with support from Juneteenth Productions.
Executive Producers: Judith McCray and Maurice Bisaillon. Senior Producer: Mary Hall. Operations & Digital Manager: Nicole Nir. Head of Development: Alina Panek. Sound Design: Erisa Apantaku & Will Jarvis.
Follow us wherever you get podcasts, or at changeagentsthepodcast.com. Subscribe to our newsletter at bit.ly/change_agents_newsletter.
Change Agents The Podcast
(Swahili) Always On: The work of resettlement
Use Left/Right to seek, Home/End to jump to start or end. Hold shift to jump forward or backward.
Wakati Wote: Kazi ya Makazi (Always On: The Work of Resettlement)
Baada ya kukimbia Uganda ili kuepuka kifungo cha maisha kwa sababu ya utambulisho wake, Adam aliwasili Chicago akiwa hana kitu isipokuwa uzoefu wake wa kazi ya kijamii. Leo hii, anahudumu kama daraja muhimu kwa wahamiaji wa LGBTQ+ wanaokabiliana na kiwewe, urasimu, na hofu zile zile alizowahi kukumbana nazo. Hadithi hii inachunguza jinsi utafutaji wa amani wa mtu mmoja ulivyokuwa utume wa saa 24 kuhakikisha hakuna mwingine anayelazimika kupitia mchakato wa makazi peke yake.
Katika hadithi hii ya sauti, tunachunguza makutano ya uhamiaji wa kimataifa na haki za LGBTQ+ kupitia sauti za wanajamii walioathirika moja kwa moja na wataalamu wa makazi. Inajumuisha mahojiano na Adam, maelezo ya kihistoria kuhusu sheria za enzi za ukoloni, na ripoti kutoka mstari wa mbele wa makazi jijini Chicago.
Imetayarishwa na Nadia Carolina Hernandez [@naddixo] kwa ajili ya Reparations Media NFP | Kwa ushirikiano na HIAS (Hebrew Immigrant Aid Society) [@HIASrefugees]
###
After fleeing Uganda to escape a life sentence for his identity, Adam arrived in Chicago with nothing but his background in social work. Today, he serves as a vital bridge for LGBTQ+ migrants navigating the same trauma, bureaucracy, and fear he once faced. This story explores how one person’s search for peace became a 24/7 mission to ensure no one else has to navigate the resettlement process alone.
In this audio story, we explore the intersection of global migration and LGBTQ+ rights through the voices of directly impacted community members and resettlement experts. Featuring interviews with Adam, archival context on colonial-era laws, and reporting from the resettlement frontlines in Chicago.
Produced by Nadia Carolina Hernandez (@naddixo) for Reparations Media NFP | In collaboration with HIAS (Hebrew Immigrant Aid Society) (@HIASrefugees)
Adam: [00:00:00] Wanataka kuniona kwamba niko na mchumba ama najitayarisha kupata mchumba ama mtoto. Hii yote ina-- wanaona kama inafanyika. Halafu maswali inakuja mingi kama hawaoni kitu yoyote.
Nadia: [00:00:19] Huyo ni Adam aliezaliwa Uganda. Adam alituomba tusitumie jina lake halisi. Anazungumzia utamaduni wa jadi wa kuingia utu uzima katika mji aliko kulia. Utamaduni unaokuja na matarajio kuhusu ndoa na familia. Na pale matarajio hayo yanaposhindikana kutimizwa, jamii huanza kuhoji. Adam alizaliwa Uganda na aliishi huko hadi mwaka wa elfu mbili kumi na saba. Anaeleza kuwa alipokuwa kijana mwenye mwelekeo wa mapenzi ya jinsia moja, alikumbana na uchunguzi mkali na hatari kutoka kwa familia yake na jamii.
Adam: [00:01:20] Wakielewa kwamba uko kwa jinsia ya kimapenzi ya watu wa sehemu moja. Hiyo inamaanisha kwamba utatupwa nje ya familia yako.
Nadia: [00:01:35] Mimi ni Nadia Carolina Hernandez na hii ni podcasti ya Change Agents. Jioni moja, alipokuwa anarudi nyumbani, Adam alimuona mwanamke anayemjua akiwa amezingirwa na kundi la wanaume. Walikuwa wakimpigia kelele na kutumia mwelekeo wake wa kimapenzi kumtisha.
Adam: [00:02:10] Ahm, hawa watu walikuwa wanaelewa kidogo kuhusu jinsia ya mapenzi ya huyu mama, ahm, si jinsia moja. Walikuwa wanampitisha vibaya, kumuongelea na sauti kubwa. Walikuwa wanataka kumuonyesha kwamba wao ni wanaume na yeye ni mwanamke ambaye anatakana apende wanaume. Mambo yalikuwa yanaenda kuwa mbaya sana.
Nadia: [00:02:36] Hali ilikuwa inazidi kuwa hatari. Adam aliingilia kati kusaidia. Alijaribu kuwavuruga wanaume wale ili kumpa yule mwanamke nafasi ya kutoroka.
Adam: [00:02:53] Nilikuwa naelewa kwamba naweza watenganisha halafu nione kama mama anaweza toroka.
Adam: [00:03:18] Watu wengi walionekana hawajali sana kitu ambaye ilikuwa inaendelea. Lakini mambo yalikuwa mbaya.
Nadia: [00:03:29] Kwa nini wanaume wale walionyesha ukali kiasi hicho? Nini kingeweza kutokea kama asingeingilia kati? Na kwa nini matukio kama haya mara nyingi hukuuzwa? Sheria ya adhabu ya Uganda iliorithiwa kutoka utawala wa kikoloni wa Waingereza iliharamisha mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja hata kwa makubaliano, ikiita vitendo hivyo mahusiano kinyume na maumbile na vitendo vya aibu. Masharti haya yalikuwa na adhabu kali hadi kifungo cha maisha. Kadri mashaka yao yalivyozidi kuongezeka, hatimaye Adam alikataliwa na familia yake. Alijikuta katika njia panda na akaanza kujiuliza kuhusu maisha yake ya baadaye nchini Uganda. Adam alihisi kutishiwa na serikali na kuachwa na familia yake pamoja na jamii. Alifanya uamuzi mgumu wa kuondoka Uganda akakimbilia kambi la wakimbizi jijini Nairobi. Adam alisomea ustawi wa jamii nchini Uganda na alitumia mafunzo hayo katika kambi la wakimbizi. Aliwasaidia wengine kujaza fomu na kutafsiri kwa ajili ya wasimamizi wa kesi. Mwaka wa elfu mbili kumi na saba, Adam aliwasili nchini Marekani na kuanza maisha Chicago. Ila haikuwa rahisi kuzoea. Alipata changamoto kupata kazi na kuzoea mazingira ya jiji. Pia alikuwa amebeba majeraha ya nafsi kutoka maisha yake ya nyuma. Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi Nilimsaidia Adam kuhama. Akiwa sasa nchini Marekani, nilimsaidia kupata kazi yake ya kwanza kama msimamizi wa kesi kwa wakimbizi kama yeye. Kadri muda ulivyopita, Adam alianza kupata utulivu na amani kwa kiasi fulani.
Adam: [00:06:27] Kwa muda ambaye nilianza kutumikia kazi kwa watu wa kijiji, hapo ndio nianza kujiangalia nyuma kuelewa kwamba mambo haiko sawa.
Nadia: [00:06:41] Kwa miaka miwili iliyopita, Adam amekuwa akifanya kazi kama mkurugenzi wa makazi mapya katika Hebrew Immigrant Aid Society, shirika la kimataifa la kibinadamu la Kiyehudi. Anawasaidia wahamiaji wapya kutoka sehemu mbalimbali za dunia kukidhi mahitaji ya msingi kama kodi ya nyumba, chakula na kupata kazi. Pia anawaongoza katika mchakato wa kuanza maisha mapya ambayo yeye mwenyewe alipitia kwa ugumu. Wateja wa Adam wanatoka pande zote za dunia. Wengi wao, kama yeye, ni sehemu ya jamii la LGBTQ. Wanakuja Marekani wakitafuta usalama, lakini mara nyingi hubeba hofu zile zile walizokuwa nazo nyumbani.
Adam: [00:08:01] Natumika kazi na watu wa jinsia moja ya mapenzi ama ambayo wanaitwa LGBT, kutoka nchi mingi, kutoka nchi ya Haiti, nchi ya Afrika, watu wengine wanatoka kwa nchi la Kiafuganistani na nchi ya Iraq pia.
Nadia: [00:08:24] Msukumo wa Marekani wa kuchukua hatua kali dhidi ya watu wasio na nyaraka halali umeifanya hofu kuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Hata wakimbizi na wanaoomba hifadhi ambao kisheria wanalindwa dhidi ya kufukuzwa nchini, wanahofu kwamba wanaweza patikana na maafisa wa uhamiaji. Mfululizo wa amri za kutoka Washington umeacha jamii nyingi bila uhakika wa haki zao.
Adam: [00:09:11] Nilipata simu mingi sana kutoka kwa hawa watu wa jinsia moja, wengine ambayo walikuwa nauliza kama warudi kasi siku ijayo ama warudi kwao kwa sababu walikuwa wanasikia mambo mengi sana. Hawa walikuwa watu kutoka Haiti.
Nadia: [00:09:31] Adam anaona watu wanaotaka kuzungumza lakini wanajizuia, wakihofia kuachilia ulinzi wao. Anajaribu kutuliza hofu zao huku akiwaunganisha na huduma zinazoweza kuboresha maisha yao.
Adam: [00:09:55] Nilikuwa naelewa kwamba hawa watu wa jinsia moja wako hapa kwa kisheria, lakini nilikuwa naangalia wameokopa sana.
Nadia: [00:10:05] Kutokana na siku zake za mwanzo Chicago, Adam anajua kwamba kuwa na mtu wa kukusaidia, mtu ambaye unaweza kumpigia simu wakati wowote, mchana au usiku, kunaweza kufanya mabadiliko magumu kuwa rahisi kidogo.
Adam: [00:10:30] Simu yangu ya kazi inapatikana ama inakuwa inapatikana kwa kila saa. Haiko kama ya wenzangu kwa kazi ambayo inatoka saa tatu asubuhi mpaka saa kumi ya jioni. Yangu inapatikana kila saa.
Nadia: [00:10:51] Baada ya siku ya kuwasaidia wengine kukabiliana na hofu na kutokuwa na uhakika, Adam mara nyingi hutembea kando la ziwa akijipa nafasi ya kupumua na kutafakari.
Adam: [00:11:13] Nikikuwa nimechoka sana na kazi ya kiakili, kwa kupumzika kwangu natembea kando ya bahari hapa Chicago, ninapata baridi inaniiingia sana vizuri halafu napumzika kiakili sana, sana.
Close: [00:11:30] Thank you for joining Change Agents, the podcast series looking at grassroots actions and solutions through stories told from the inside out. Change Agents is produced by Reparations Media. The music is composed by Sarah Abdulla. Funding support is provided by the Chicago Community Foundation, the Chicago Community Trust, the Field Foundation, the Wayfarer Foundation, and the Lumpkin Family Foundation. Subscribe to this podcast on Apple Podcasts, Spotify, Stitcher, and wherever you find podcasts. And follow Change Agents on Facebook, Instagram, and our website, changeagentsthepodcast.com.